Saturday

WASOMI WETU NA MAADILI YA TANZANIA

NACHUKUA NAFASI HII ADHIMU KUMSHUKURU MOLA KWA AFYA NA UZIMA ALIONIPA, NI SIFA ZAKE POMONI, NA PIA NAWATAKIA KHERI TENGAMAVU WATANZANIA WOTE. MOYO UNANISHAWISHI NIYASEME YALIYO NA UKWELI, NANYI PIA NAOMBA MITAZAMO YENU.

KWA HAKIKA MAADILI YA MTANZANIA YAMEHARIBIWA NA YANAENDELEA KUHARIBIWA NA TABAKA LINALOJIITA WASOMI , NIMEJARIBU KUFIKIRI KITUNDUIZI NIKAMEGUNDUA MAMBO MBALIMBALI KWA HAKIKA NANYI MTAWEZA KUTEKENYEKA HISIA ZENU NA MKANIPATIA MAWAZO YALIYO BAINIFU.

UTOAJI WA MIMBA KWA WASICHANA NA WANAWAKE , WASOMI WETU WANAHUSIKA NA HAYA NI MAADILI MABAYA YANAYOSABABISHWA NA HAWA WASOMI.

SUALA LA UFISADI KWA BAADHI YA VIONGOZI WETU NALO PIA WASOMI WETU WANAHUSIKA KWA MAANA VIONGOZI NI HAOHAO WASOMI. JE HAYO SI MAADILI MABAYA?

SUALA LA RUSHWA KWENYE SEKTA ZA KIJAMII NALO PIA WASOMI WETU WANAHUSIKA.

UTUMIAJI WA VILEVI HASA MADAWA YA KULEVYA WASOMI WETU WANABIDI WAULIZWE NA WAWAJIBIKE KWA HILO.

WIZI WA MITIHANI NALO PIA LINASABABISHWA NA UWEPO WA WASOMI WETU,JE ELIMU ITATUKUMBOA KIUCHUMI?

MAVAZI YALIYO NUSU UCHI NA PENGINE UCHI KABISA KWA BAADHI YA DADA ZETU KATIKA VYUO VYETU VIKUU NALO PIA WASOMI WETU WANAHUSIKA NA NDIO CHANZO HALISI CHA UPOTEVU WA UTU, HESHIMA NA MAADILI KWA MTANZANIA.

MATUMIZI MABOVU YA NGAMIZI (COMPUTER), HASA WANAOPENDA KUANGALIA PICHA ZA NGONO, HAPA NASEMA WAZI WAZI KWA MAANA WASOMI WENGI NDIO WANAOHUSIKA NA HILI HASA WANAFUNZI WA SEKONDARI HADI VYUONI.

KUKOSEKANA KWA AMANI, KUSHUKA KWA UCHUMI WETU NI WASOMI HAOHAO NDIO WANAHUSIKA.JE TUTAFIKA?

MWISHO, NAPENDA KUAMINI WASOMI WENGI WANAANZA KUBADILIKA WAKIWA VYUO VIKUU AMBAPO KUNAPELEKEA KUJITOKEZA KWA MAADILI MABAYA MIONGONI MWA JAMII YETU YA TANZANIA,JARIBU KUMUANGALIA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHOCHOTE, KABLA HAJAENDA HUKO ALIKUWA VIPI? NA BAADA YA KWENDA YUPO VIPI?NA ANAPOMALIZA CHUO ANAKUWA VIPI?

HAYA YOTE NILIPATA KUYAONA KATIKA VYUO VIKUU MBALI MBALI NILIVYOPATA KUVITEMBELEA HAPA NCHINI, AMBAPO KILA KUKICHA VINAZIDI KUONGEZEKA. NATUMAINI KWA DHATI YAKE NIMEWEZA KUWATEKENYA NANYI PIA MMETEKENYEKA VYA KUTOSHA.
HAWA NDIO WASOMI WETU WA TANZANIA

TUKUMBUKE KUWA MTEGO HUNASA WALIOMO NA WASIOKUWEMO, hebu rejea hadithi hii ya zama zile za akina bibi na babu.

Hapo zamani za kale palikuwepo na panya, kuku, , mbuzi na ng’ombe. Panya akawalalamikia wenzake, akaanza na kuku akisema, “Hapa kijijini tulipo kuna mtego unawamaliza panya sisi akina panya tunakwisha, tusaidieni.” Lakini jibu la kuku lilikuwa hivi, “Hilo halinihusu.” Panya hakukata tamaa bali alimwendea mbuzi na kumpa kilio kilekile. Cha ajabu jibu la mbuzi lilikuwa hivi, “sina nafasi na mambo madogo kama hayo.” Panya hakuchoka, alimwendea ng’ombe na kumpa hoja ileile. Jibu la ng’ombe lilikuwa, “Nenda kafie mbali na siku nyingine usinieleze upuuzi kama huo''Ikafika siku, katika sehemu wanapoishi wote panya, kuku, mbuzi, na ng’ombe, akapita nyoka na kunasa kwenye mtego na kotofanikiwa kutoka. Huku akidhani ni panya, mama mwenye nyumba akapeleka mkono kwenye mtego. Lahaula! Nyoka yule mwenye sumu akamng’ata na mama yule ghafla akaugua sana. Katika kufanya matibabu ikaonekana mgonjwa anahitaji supu na supu ilioonekana nzuri kw mgonjwa ni supu ya kuku. Kuku akachinjwa yuleyule aliyesema mtego haumuhusu. Mama yule hakupata ahueni hivyo akaenda kwenye matibabu ya pesa nyingi. Mbuzi akauzwa ili pesa ipatikane. Aliyemnunua mbuzi ni mchoma nyama na mpika supu, mara baada ya kumnunua alimchinja mbuzi yule kwa ajili ya supu na mishikaki na ni yule yule mbuzi alisema hana nafasi na mambo madogo kama mtego wa panya. Hatimaye mama yule alifariki dunia na watu wengi walikwenda kwenye msiba. Hivyoikaamuriwa ng’ombe achinjwe kwa ajili ya kitoweo. Ng’ombe alichinjwa na ni yuleyule ambaye hataki kuelezwa upuuzi kama mtego wa panya.

JAMANI TUKUMBUKE KUSADIANA KWENYE SHIDA, RAHA NA MATATIZO YASIJE YAKATUKUTA YA KINA MBUZI, NG'OMBE NA PANYA.

No comments:

Post a Comment