NACHUKUA NAFASI HII ADHIMU KUMSHUKURU YEHOVA KWA KUNIFIKISHA HAPA NILIPO, NI SIFA ZAKE POMONI, NA PIA KUWATAKIA KHERI TENGAMAVU WATANZANIA WOTE KWA MWAKA 2008. MOYO UNANISHAWISHI NIYASEME YALIYO NA UKWELI, NANYI PIA NAOMBA MITAZAMO YENU. KWA HAKIKA MAADILI YA MTANZANIA YAMEHARIBIWA NA YANAENDELEA KUHARIBIWA NA TABAKA LINALOJIITA WASOMI , NIMEJARIBU KUBWABWASA KITUNDUIZI NA NIMEGUNDUA MAMBO MBALIMBALI KWA HAKIKA NANYI MTAWEZA KUTEKENYEKA HISIA ZENU NA MKANIPATIA MAWAZO YALIYO BAINIFU.
HOJA ZANGU NI:
UTOAJI WA MIMBA KWA WASICHANA NA WANAWAKE , WASOMI WETU WANAHUSIKA NA HAYA NI MAADILI MABAYA YANAYOSABABISHWA NA HAWA WASOMI.
SUALA LA UFISADI KWA BAADHI YA VIONGOZI WETU NALO PIA WASOMI WETU WANAHUSIKA KWA MAANA VIONGOZI NI HAOHAO WASOMI. JE HAYO SI MAADILI MABAYA?
SUALA LA RUSHWA KWENYE SEKTA ZA KIJAMII NALO PIA WASOMI WETU WANAHUSIKA.
UTUMIAJI WA VILEVI HASA MADAWA YA KULEVYA WASOMI WETU WANABIDI WAULIZWE NA WAWAJIBIKE KWA HILO.
WIZI WA MITIHANI NALO PIA LINASABABISHWA NA UWEPO WA WASOMI WETU,JE ELIMU ITATUKUMBOA KIUCHUMI?
MAVAZI YALIYO NUSU UCHI NA PENGINE UCHI KABISA KWA BAADHI YA DADA ZETU KATIKA VYUO VYETU VIKUU NALO PIA WASOMI WETU WANAHUSIKA NA NDIO CHANZO HALISI CHA UPOTEVU WA UTU, HESHIMA NA MAADILI KWA MTANZANIA.
MATUMIZI MABOVU YA NGAMIZI (COMPUTER), HASA WANAOPENDA KUANGALIA PICHA ZA NGONO, HAPA NASEMA WAZI WAZI KWA MAANA WASOMI WENGI NDIO WANAOHUSIKA NA HILI HASA WANAFUNZI WA SEKONDARI HADI VYUONI.
KUKOSEKANA KWA AMANI, KUSHUKA KWA UCHUMI WETU NI WASOMI HAOHAO NDIO WANAHUSIKA.JE TUTAFIKA?
MWISHO, NAPENDA KUAMINI WASOMI WENGI WANAANZA KUBADILIKA WAKIWA VYUO VIKUU AMBAPO KUNAPELEKEA KUJITOKEZA KWA MAADILI MABAYA MIONGONI MWA JAMII YETU YA TANZANIA,JARIBU KUMUANGALIA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHOCHOTE, KABLA HAJAENDA HUKO ALIKUWA VIPI? NA BAADA YA KWENDAYUPO VIPI?NA ANAPOMALIZA CHUO ANAKUWA VIPI?
HAYA YOTE NILIPATA KUYAONA KATIKA VYUO VIKUU MBALI MBALI NILIVYOPATA KUVITEMBELEA HAPA NCHINI, AMBAPO KILA KUKICHA VINAZIDI KUONGEZEKA. NATUMAINI KWA DHATI YAKE NIMEWEZA KUWATEKENYA NANYI PIA MMETEKENYEKA VYA KUTOSHA.
HAWA NDIO WASOMI WETU WA TANZANIA