Saturday

ANGALIA UNACHOWEZA KUFANYA

TAARIFA YA SHULE YA AWALI, AMANI,DODOMA INAYOFUNDISHA WATOTO WENYE VIRUSI VYA UKIMWI,YATIMA NA MATATIZO MBALIMBALI

Shule ya Amani ilianzishwa mwaka 2004 kwa madhumuni ya kufundisha elimu ya awali kwa watoto wenye matatizo yafuatayo : -

*
watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi
*
watoto yatima
*
watoto wanaotokea katika mazingira magumu
*
watoto wasiojiweza kiuchumi na kijamii.

Shule hii ya amani ilikuwa inafadhiliwa na shirika la kujitegemea linaloitwa TUNAJALI ambalo linajishughulisha na kuhudumia wagonjwa wa ukimwi katika vituo mbali mbali na majumbani. Kwa sasa kituo hiki kinaendesha shughuli zake katika kanisa la ANGILIKANA ambalo lipo MAKOLE(Dodoma) chini ya mchungaji Omary Malilo. Kwa muda wa miaka miwili sasa shule hiki hakina mfadhili kutokana na shipika la TUNAJALI kuacha kudhamini shule hii na kujikita zaidi kwa wagonjwa wa majumbani. Toka kujitoa kwa wadhamini hawa shule hii haina mdhamini yoyote aliyejitokeza kusaidia ukiacha wasamalia wema na kanisa ambao husaidia mara moja moja. Shule hii ina jumla ya watoto 150 ambapo 31 wanasoma shule hii ya awali na 119 wanasoma shule za msingi na sekondari katika mkoa wa Dodoma. Watoto ambao wapo shuleni hadi sasa ni :-

1. WIDO SADD - Muathirika
2. LAURENT MAZENGO - Muathirika
3. IDD SOGORAC - Ana moyo mkubwa wenye tundu
4. KULWA KASSAND - Hana baba
5. DOTTO KASSANDA - Hana baba
6. EDISON MTERA - Hana baba
7. HASHIRI JUMA - Hana baba
8. REHEMA NGOMOKA - Hana baba
9. CHRISTIAN LEONARD - Hana baba
10. LEONARD MAGOMA - Hana baba
11. FRANK VISENT - Hana baba
12. ASHA MUSSA - Hana baba
13. EMMANUEL RAGUNA - Hana baba
14. ROMAN DANIEL - Mama kipofu
15. WILLY DANIEL - Mama kipofu
16. MAGINGA MASAKA - Mama tahira
17. JANE SHEDRACK - Baba kipofu
18. ZUBEDA - Mazingira magumu
19. BLAYANI LUMBILA - "
20. MICHAEL CLAUD - "
21. CECY MWINJE - "
22. JOSEPH MARK - "
23. FRANCE PAUL - "
24. KULWA CHALRES - "
25. DOTTO CHARLES - "
26. TATU KARAMA - "
27. BOSTON MAHOMA - "
28. ISABELA CHANKALI - "
29. MOSES MAGODA - "
30. HOSIANA MALODA - "
31. EMANUEL REGUNA - "

Watoto wote hawa wanahudumiwa na watu watatu tu ambao ni :-

1. LAURENCIA AUGUSTO CHAWALA - Mwalimu
2. MONICA LEONALD MAHOMA - Mwalinu
3. KAUNDIME MUSSA - Mpishi na Msafishaji

Wahudumu hawa wanaishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa mishahara kwa muda wa miaka miwili japokuwa hapo awali walikuwa wanalipwa shilingi 5000 kwa mwezi. Miaka yote miwili wahudumu hawa walikuwa wanajitolea. Wahudumu hawa wanaomba wafadhili wawasaidie mambo yafuatayo :-

* wanaomba kupewa mishahara mizuri kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu kila kukicha. Wanaomba kulipwa 40,000 hadi 80,000 kadri itakavyowezekana kutokana na kupanda kwa gherama za maisha.
* kusaidiwa unga kilo 25 na sukari kilo 15 kwa ajili ya uji wa watoto kila mwezi.
* kusaidiwa vifaa mbalimbali vya wanafunzi kama kalamu, madaftari, mabegi na sare za shule.


Wahudumu hawa wanaomba msaada wako(wenu) kwa hali na mali. Wanatanguliza shukrani zao za dhati na wtashukuru kwa msaada wowote utakaowasaidia.

Kwa masiliano zaidi wasiliana nao kwa namba 0755931568 au nenda kawatembelee kanisa la ANGLIKANA, MAKOLE. Wanaatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
David Harrison Chinyuka
0713939326, 0767939326
djharr85@yahoo.com, dahachi@live.com