Thursday

WHAT HAS HAPPEN TO LOVE

WATU NA FALSAFA YA MAPENZI

Suala la mapenzi linawasumbua watu wengi sana hasa vijana ambao ndio kwa kiasi kikubwa wamejikita zaidi katika mahusiano ya mapenzi hasa pindi wanapotafuta mtu wa kuishi nae katika maisha.

Suala la mapenzi limejadiliwa na watu mbalimbali katika vitabu,magazeti,vitini na vyombo vya habari ambavyo kwa kiasi kikubwa vinapotosha maana halisi ya mapenzi kwa kuzungumzia mambo ambayo kiuhalisia hayawezekani.
Mfano wa vitabu kama:-

· Jinsi gani unaweza kumpata mchumba wa kweli
· Lets talk about love sex and marriage
· Msinyimane

Na vitabu vingine vingi. Najua kuwa hapa vijana wengi watakuwa wanajua vitabu vingi zaidi. Vijana wenzangu ninachotaka kuwaambia ni kwamba, msitegemee sana vyombo vya habari au magazeti na vitabu ili kuweza kuanzisha au kujenga uhusiano na msichana au mvulana maana ni lazima itakuletea matatizo hapo baadae.

Vitabu vingi ,magazeti yanayohusu mapenzi pamoja na tamthiliya zinatengenezwa kwa lengo la kukuburudisha wewe msomaji na kuwapa faida wale wanaotengeneza na kuandaa mambo hayo, huku wewe msomaji na mtazamaji ukipata faida ndogo sana kwani mambo mengi yanayozungumziwa hayana uhalisia maana ni mara chache sana kutokea katika jamii ya sasa iliyojaa mafisadi ambao wanajiita wasomi.

Vijana kumbukeni kuwa mapenzi ya kweli na ya dhati huwa hayapatikani kirahisi.Mara nyingi vitabu vya mapenzi,taamthiliya,magazeti na filamu huleta gharama kubwa katika moyo wa mhusika kutokana na hisia kali anazozipata mtu baada ya mambo kwenda kombo au kinyume na vile mtu huyo alivyotarajia.

Vijana mpo hapo,hasa walei mnaojiita wasomi au wengine husema kizazi cha .com(doti komu). Kuweni makini sana na mambo haya vijana kwa maana 65% ya vijana hutumia muda wao mwingi kufanya mambo haya:-
Kusoma vitabu vya mapenzi vyenye kuvuta hisia za matamanio
Kuangalia filamu na tamthiliya za mapenzi
Kuangalia picha za ngono katika mtandao

Hivi mnajifunza nini kutokana nna mambo haya? Au ndio kupata mitazamo ya kidhanifu kuhusu suala la mapenzi na kwenda mojamoja kuyafanyia kazi bila kufanya uchunguzi wa kina.Msidanganyike kaka zungu,dada zangu,mama zangu,baba zangu na wadogo zangu, jiulize swali la msingi. Hivi ni kweli picha za ngono,filamu pamoja na tamhiliya za mapenzi,vitabu, magazeti,vipindi vinavyohusu mapenzi katiaka radio na luninga ndio suluhisho lakumfanya mtu kuanzisha uhusiano .Kujikita katika masuala haya kumuwafanya vijana wengi kujiingiza katika mapenzi na kujikita katika uga huu wakiwa na umri mdogo kabisa.

Utakuta kijana wa miaka 12 hadi 18 anakudadafulia kuhusu suala la mapenzi kama vile ni mwalimu mzoefu kuwazidi hata watu wazima. Ukimuuliza kijana wa namna hii kuhusu elimu hii ya mapenzi atakujibu kuwa ameipata kutoka katika vitabu,magazeti na majarida ya mapenzi,tamthiliya,picha za ngono,filamu,miziki na mambo mingine ambayo ni mara chache huwa yanazungumzia ukweli kuhusu mapenzi.

Jamani hebu tuwe makini sana na masuala haya maana yana athari kubwa kisaikolojia na katika maisha kwa ujulma. Suala la msingi ni kuweza kutofautisha kati ya uongo na ukweli,kitu halisi na kisicho halisi. Hebu tuamke na tutofautishe mapenzi ya ukweli na halisi na yale yasio ya ukweli, mapenzi ya kuandikwa,kuimbwa,kuigizwa na kuangaliwa.

HEBU TUWE MAKINI NA MAMBO HAYA MAANA UKIHARIBU SASA BAADAE UTAREKEBISHA KWA MBINDE SANA.

WAHENGA WALISEMA

KWA KAWAIDA TAMU HAIDUMU KWANI IKIDUMU HUISHA HAMU.